IJUE HUKUKUWASHU
(HUDUMA YA KUWAANDAA NA KUWAPELEKA WATENDAKAZI SHULENI)
UTANGULIZI
Mpendwa mtumishi wa
Mungu, nakusalimu katika jina kuu la Yesu Kristo.
Natumia nafasi hii kukukumbusha kuwa wewe ni mtumishi
maalumu wa Mungu kama Bwana akuonavyo.
Mungu amekuchagua ili uweze kutikisa ulimwengu na kuvunja
nguvu za utawala wa giza
kupitia mamlaka ya neno lake.
Kama mtumishi wa Mungu aliye mkuu sana Muumba mbingu na nchi, usiangalie
upungufu ulio nao, bali angalia kile ulicho nacho. Kwa sababu Mungu amekupa
kitu ambacho wengine hawanacho, na njia kuu ya mafanikio ni pale Mungu
anapokutumia kuleta uamsho kukuwezesha kufikia bkusudi lake alilokuitia.
HISTORIA
HUKUKUWASHU:
Ina lengo la kuwawezesha watumishi wenye shauku ya
kuwafikia vijana shuleni na vyuoni kwa kuwapa elimu. Kuwaunganisha ili waweze
kufikia malengo yao
ya kuleta uamsho na kuwaleta vijana na wasomi wengi kwa Yesu.
Huduma shuleni na vyuoni ni huduma ambayo imeanza miaka
mingi kwa mtu mmoja mmoja kupokea wito na mzigo wa kuwafikia vijana na
wanafunzi.
Mwaka 2012 Mungu aliweka mzigo ndani ya watumishi
waliokuwa wakifanya huduma shuleni na vyuoni, mmoja wao akiwa Awaichi Sahara wa
kuanzisha mtandao wa kudumu kwa wanafunzi shuleni na vyuoni.
Mtandao huu ulianza kukutana mara ya kwanza tarehe
17.03.2012. Na walikutana watumishi na wahudumu shuleni na vyuoni wapatao 55,
ambao walitoka katika makanisa 16 ambayo ni mchanganyiko wa madhehebu
mbalimbali wakiwemo wachungaji watano na waalimu wa huduma shuleni na vyuoni wapatao 50.
MAKUSUDI:
- Kuwaandaa, kuwatia moyo na kuwaunganisha watumishi watakao wafikia vijana na wanafunzi shuleni na vyuoni.
- Kuwajenga na kuwainua watumishi wa kiroho ili waweze kufikia lengo la kuujenga na kuufikia ufalme wa Mungu.
- Kutafuta wawezeshaji; kuandaa semina, makongamano na majadiliano mbalimbali yatakayowainua wanaume na wanawake watakaoleta mabadiliko kwa vijana walioko shuleni na vyuoni.
- Kuyahimiza makanisa na wachungaji ili kuona hitaji lililopo la kuwafikia vijana katika shule za msingi, sekondari na vyuoni ili kuweza kutimiza agizo kuu.
- Kuandaa mitaala ya kufundishia.
- Kufanya utafiti na tathimini, ili kujua shule zilizo na uhitaji wa wahudumu.
MAONO
Ni kuwasha moto na kuleta uamsho ndani ya makanisa na
kuleta umoja utakaosababisha injili kuhubiriwa katika shule na vyuo na
kuwafanya wanafunzi wamjue Yesu Kristo Bwana na mwokozi wao na kujio
kumtumikia.
UTUME
HUKUKUWASHU; Itawatambua, itawatia moyo, kuwahiza na
kuwawezesha washirika na watumishi wa makanisa mbalimbali kwa kuwapa mafunzo na
kuwafanya waungane kutimiza agizo kuu kwa wanafunzi shuleni na vyuoni.
MKAKATI
- Kuwakumbusha wachungaji na viongozi wote wa makanisa kuwaandaa na kuwahimiza washirika na makanisa yao ili wazifikie shule na vyuo vyote vilivyo katika maeneo yao.
- Kuandaa semina,makongamano na mijadala mbalimbali katika kata, wilaya na mkoa ya kuwaandaa watumishi watakaojitelea kwa huduma shuleni na vyuoni.
- Kuandaa vikao vya wachungaji vya wahudumu wa vijana wa shuleni na vyuoni, kila baada ya miezi miwili ili kupokea taarifa na kujadili changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo wahudumu wa vijana shuleni na vyuoni.
- Kuandaa na kukubaliana juu ya mitaala itakayotumika kufundisha vijana wetu katika shule na vyuo.
- Kuweka utaratibu maalumu wa kumuomba Mungu apelike watendakazi wenye maono na mzigo wa kuwafikia vijana shuleni na vyuoni.
- Kuyakumbusha makanisa kuandaa bajeti na kuweka mipango ya kuwezesha kifedha huduma za shule na vyuoni.
- Kuwahimiza wahudumu wa huduma mashuleni na vyuoni wawe chachu ya kuwaandaa washirika wenzao kuwa na utayari wa kufanya huduma shuleni na vyuoni.
Kwa mawasiliano:
Mratibu HUKUKUWASHU
Awahiche Sahara
Simu +255-754-673-399
Arusha, Tanzania
E-mail; ggideon77@yahoo.com
No comments:
Post a Comment